www.kenethngamoga.blogspot.com

Instagram kuanza kutumia nembo mpya

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa. 

Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua. Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika mtandao wa Instagram, mtandao huo una takriban wateja milioni 400 na uliipiku Twitter mwaka 2014.
Viongozi wa mtandao wa Instagram waliiambia Newbeat, “Wakati Instagram ilipokuwa inaanza ilikuwa na eneo la kukarabati na kusambaza picha. Miaka mitano baadaye likawa ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video.”
Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe. Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo. Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita.
Aidha walitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment