Akielezea tukio hilo muhudumu wa nyumba ya kulala wageni Ester Mshimika amesema mwanaume ambaye alikuwa amelala moja ya vyumba vya nyumba hiyo kuondoka bila kuaga wakati ndani akiwa amemuacha mwenzake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei
Akielezea tukio hilo muhudumu wa nyumba ya kulala wageni Ester Mshimika amesema mwanaume ambaye alikuwa amelala moja ya vyumba vya nyumba hiyo kuondoka bila kuaga wakati ndani akiwa amemuacha mwenzake.
Amesema baada ya muda mrefu kupita aliamua kumgongea aliyebaki ndani bila kuitika ndipo aliamua kumuita meneja wake na kisha kutoa tarifa kwa jeshi la polisi hadi walipofika na kukuta mwanamke huyo amekwisha fariki dunia huku mwenzake akiwa ametokomea kusiko julikana.
Mganga wa zamu katika hospitali ya mtakatifu Fransisco ya mjini Ifakara Dkt. Isaya Msumba amekiri kupokea mwili wa mwanamke huyo ambapo amesema uchunguzi unaonyesha marehemu alichomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kukata mshipa mkubwa wa kupeleka damu kichwani na moyoni hivyo kusababisha damu kuvuja nyingi na hivyo kupoteza maisha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea mauaji hayo ya kikatili na kwamba jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kumtafuta kijana wa kiume anayedaiwa kutekeleza mauaji hayo kwani imebainika kuwa alikuwa mfanyabiashara mwenzake wa mazao.
0 comments:
Post a Comment