www.kenethngamoga.blogspot.com

Wema Sepetu asema yeye ni dhahabu inayogombewa na watu, hajali wanao mchafua

Mrembo wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, amesema yeye ni dhahabu inayogombewa na watu hivyo hajali hata kama atachafuliwa namna gani katika mitandao ya kijamii.
Wema aliliambia MTANZANIA kwamba, hana mpango wa kujibu vibaya vinavyoongelewa kuhusu yeye kwa kuwa yeye bado ni dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu.
“Mimi ni kama dhahabu hivyo kila mtu anatamani kuishika, watu wanaacha kufanya yao kila siku Wema, kwa sasa niko na mambo yangu ya kutafuta fedha sina habari na mtu hata aniandike vibaya vipi,” alisema Wema.
Aliongeza kwamba licha ya kusemwa, amezidi kujiongezea mashabiki na mikataba mbalimbali ya kufanya kazi na makampuni yenye majina makubwa kwa kuwa yeye ni kama dhahabu isiyochafuka.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment