www.kenethngamoga.blogspot.com

UTAFITI: Wanasayansi wamegundua mnyama mwenye ubongo sawa na binadamu

Utafiti mpya uliyofanywa na Chuo Kikuu cha New York, Marekani umegundua mnyama mwingine ambaye ana ubongo mkubwa sawa na binadamu ambapo utafiti huo ulionesha jinsi gani mazingira wanayoishi binadamu na Nyani yanavyoshabihiana na kuwafanya kuwa wanyama pekee wenye ubongo ulio sawa kwa ukubwa.

Mkuu wa utafiti huo Alex Decasian alizungumza na BBC >>> “Nyani hasa jamii ya Orangutans wana ubongo ulio sawa na binadamu kwa kuwa hupitia changamoto zinazofanana, nyani mwenye umri mkubwa ana ubongo mkubwa zaidi kuliko Nyani mtoto, hii inasadia katika ulinzi wa jamii yao na kutatua matatizo kama ugomvi”
Utafiti huo pia ulionesha nyani anayekula matunda ana ubongo mkubwa zaidi ukilinganisha na nyani anayekula majani na mizizi ambapo Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha
Oxford amesema ubongo mkubwa humtofautisha nyani na wanyama wengine katika uelewa wa mambo, kuwa na huruma na kutambua majukumu yao.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment