www.kenethngamoga.blogspot.com

Trump: Sitafuta mpango wa Obamacare

Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliyefanya kampeini ya kupinga Bima ya afya inayofaahamika kama Obama care, sasa amesema atafanyia marekebisho machache kipengee cha sheria juu ya bima hiyo ya matibabu kwa gharama nafuu.
Trump amemtaja Clinton kama mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwaImage copyrightAFP
Image captionTrump amemtaja Clinton kama mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwa
Katika mahojiano ya kwanza tangu achaguliwe rais siku ya Jumanne, Trump ametangaza mageuzi makubwa ya sera punde atakapochukua nafasi ya Barack Obama katika Ikulu ya White House mwezi Januari mwaka ujao.
Bwana Trump, aliyesisitiza vikali kuwa atafutilia mbali bima hiyo inayowapa fursa mamilioni ya Wamarekani maskini kupata huduma ya afya kwa bei nafuu punde tu atakapochaguliwa rais, yaonekana amebadilisha msimamo wake juu ya suala hilo.
Na Katika kile kinachoonekana kulegeza msimamo wake juu ya mpinzani wake Hillary Clinton, Rais huyo mteule amesema,Clinton ni mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwa.
BBC SWAHILI
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment