Hatimaye imefahamika kuwa Antonio Guterres, kutoka Ureno ndiye atakayeshika madaraka ya ukatibu mkuu wa UN Januari 1, 2017 baada ya katibu mkuu wa sasa raia wa Korea Kusini Ban Ki-moon kustaafu wadhifa huo.
Inaelezwa kuwa Kamishna huyo Mkuu wa zamani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi, atakabialiana na mgogoro mkubwa tangu Vita Kuu vya Dunia. Gutteres ameteuliwa rasmi Alhamisi ya October 13, 2016 na nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kuongoza taasisi hiyo nyeti kwa miaka mitano, ikiwa ni baada ya kupokea baraka Alhamisi iliyopita kutoka nchi 15 wanachama wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Guterres amezitolea wito nchi zenye nguvu duniani kuachana na tofauti zao kuhusu Syria, wakati yakikaribia mazungumzo mapya ya kimataifa kuhusu mgogoro wa Syria ambao umewaua watu zaidi ya 300,000 na kusababisha maefu ya raia wa Syria kukimbilia nje ya nchi tangu mwaka 2001
.BBC
0 comments:
Post a Comment