Baadhi wamesema kuwa hawana uwezo wa kuzirejesha fedha hizo kwani hawakuwaomba
kufanya safari hizo kwwakuwa ilikuwa sehemu ya kazi zao kwahiyo kiasi cha fedha hizo
walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi kuwawezesha na kufika katika eneo hilo.
“Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za mbio za Mwenge wa uhuru, tuliambiwa kuja
na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa
kwasababu ilibidi tule na kulala kwenye nyumba za wageni,tutapata wapi hela za kuzirudisha,
hapo sisi kosa letu liko wapi,”? alihoji mmoja wa madereva aliliambia gazeti la The Citizen.
“Ili nibidi nilipe chumba kwa siku 7 ambazo nilitarajia kuishi hapa kama nilivyotumwa kwa uhaba wa
vyumba,sasa naanzaje kumwambia mmenyewe arudishe fedha yote ili niirejeshe ofisini ?alihoji.
Wiki iliyopita Rais John Magufuli alisitisha safari ya viongozi wa mikoa na wilaya kwenda Simiyu
kwenye kilele cha mbio za Mwenge na kuwataka wale waliokwisha chukua posho kuzirejesha.
BY: EMMY MWAIPOPO
0 comments:
Post a Comment