www.kenethngamoga.blogspot.com

MBUNGE WA KILOMBERO ''PETER LIJUALIKALI''ATOA YA MOYONI BAADA YA KUSIKIA AZMINA MBILINYI KAFUTWA KAZI NA RAISI MAGUFULI

Mbunge wa jimbo la kilombero Perter Ambosi Lijualikali jana usiku july 30 ametoa ya moyoni kwa kuandika ujumbe mzito kupitia Ukurasa wake wa facebook kwenda kwa aliekuwa mkurugezi wa jimbo la kilombero ambae ndiye aliesimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 katika jimbo la kilombero na Mlimba Bi Azmina Mbilinyi.
Katika ujumbe huo ulioandikwa na mbunge huyo anaekubalika zaidi katika ukanda huu wa pwani kwamba amesikitishwa sana na hatua zilizochukuliwa kwa kufukuzwa kazi kwa mkurugenzi huyo wa Bagamoyo ambae amedumu madarakani kwa kipindi cha siku 24 tu tangu aamishwe kutoka kilombero na kwenda Dodoma kabla ya kuamishiwa wilayni Bagamoyo alikofukuzwa kazi july 30 2016
UJUMBE HUO UNASOMEKA HIVI>>>>>>>>
""Kwako Azimina Mbilinyi
Nimekufahamu tangu nilipopata kura nyingi katika uchaguzi wa Udiwani kata ya Ifakara mwaka 2013 na aliyepaswa kunitangaza, mtendaji wa Ifakara Bw. Akley Muhenga akasita kunitangaza lakini ukaingilia kati na kunitangaza Mshindi, labda kwa sababu uliogopa wananchi wengi wangekufa kwa kipigo cha mapolisi kama nisingetangazwa.
Tumefanya kazi katika Halmashauri ukiwa Mkurugenza na mimi nikiwa diwani. Nimeshuhudia ukipewa sifa kemukemu za utendaji uliotukuka.
Mwaka 2015, Ulisimamia kwa haki uchaguzi wangu wa kugombea ubunge na ukanitangaza mshindi wa ubunge jimbo la Kilombero. Ulipoitwa mahakamani kutoa ushahidi dhidi yangu ili nizulumiwe haki yangu, uligoma kusema uongo, ulizungumza ukweli. Ulipinga kila hila mbaya walizokujaribu nazo.
Leo wamekufukuza kazi, wanasema hawaridhishwi na utendaji kazi wako. Aliyekua mgombea wa CCM jimbo la Kilombero, Abubakari Assenga anafurahia na kuchekelea kufukuzwa kwako. Huenda sijui mengi kuhusu utendaji wako lakini ninaomba nikwambie maneno yafuatayo, MUNGU NI MWEMA! Atakupigania kama umefanyiwa hila.""

Ikumbukwe kuwa mbunge huyu wa jimbo la kilombero alikuwa na kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na Aliekuwa mgombea wa ccm ndugu Abobakari Asenga na july 29 ndio ilikuwa siku ya hukumu ambapo Lijualikali alitangazwa kuwa mshindi
Pia kwa upande wa jimbo la mlimba kulikuwa na kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na Mgombea wa ccm Godwin Kunambi  dhidi ya Suzan Kiwanga na maamuzi ya mwisho ya mahakama Suzani kiwanga amepata haki na anaendelea na ubunge wake
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment