www.kenethngamoga.blogspot.com

matokeo ya kidato cha sita 2016 haya hapa

Baraza la mitihani la Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita ulofanyika mwezi May mwaka huu ambapo kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia 1.33 ikilinganmishwa na asilimia mwaka 2015
.
Akitoa matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari katibu mtendaji wa baraza hilo Bw. Charles Msonde ameeleza kuwa licha ya ufaulu kushuka lakini kiwango cha ubora wa watanhiniwa katika madaraja ya ufaulu imeongezeka, ambapo kiwango cha ufaulu kwa mwaka 2016 ni asilimia 97.32 ikilinganmishwa na asilimia 98.65 mwaka 2015.
Bw. Msonde amesema kati ya watahiniwa 74,896 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita watahiniwa 956 hawakufanya mtihani , wavulana walifaulu ni 39,466 sawa na asilimia 97.55 na wasichana waliofaulu ni 24,062 sawa na asilimia 98.59.
Aidha amezitaja shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Shule ya sekondari ya Kisimiri kutoka mkoa wa Arusha huku shule ya mwisho kitaifa ikiwa ni shule ya sekondari ya Lumumba iliyopo katika mkoa wa Unguja.
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 8,023 sawa na asilimia 92.64 ikilinganishwa na mwaka 2015 watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 4,076 sawa na asilimia 88.34 waliofaulu mtihani huo.
Msonde ameeleza kuwa ikilinganishwa na mwaka 2015, takwimu za ufaulu kimasomo zinaonesha kushuka kwa ufaulu, katika masomo ya sayansi kati ya asilimia 5.36 na 8.9, kwa upande wa masomo ya sanaa kati ya asilimia 0.00 na 4.43 na masomo ya biashara kati ya asilimia 1.7 na 6.9.
Shule 7 kutoka Unguja ni miongoni mwa zilizoshika mkia ikiwemo Azania ya jijini Dar es salaam.
Shule 10 za mwisho Mpendae, Ben bella ,Tumekuja,Green Bird Boys, Jang'ombe, Kiembesamaki, Tanzania Adventist, Ala_ihsan girl, Azania na Lumumba .
Zilizoongoza ni Kisimiri, Feza Boys, Alliance Girls, Feza Girls, Tabora Boys, Marian Boys, Kibaha, Mzumbe, Ilboru na Tandahimba
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment