www.kenethngamoga.blogspot.com

Afariki kwa kuchomwa sindano ya kutoa ujauzito

Msichana mmoja amefariki dunia baada ya kuchomwa sindano ya kutoa ujauzito na muuzaji wa dawa baridi za binadamu wilayani Kwimba mkoani Mwanza.


Taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Mwanza imeeleza kwamba tarehe 20.07.2016 majira ya saa 2:00 asubuhi katika kijiji cha Nyamatara kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza, msichana aliyejulikana kwa jina la Anna Martine miaka [18] makazi kijiji cha Matara, alifariki dunia.
Msichana huyo alifariki baada ya kuchomwa sindano ya kutoa ujauzito wa miezi 03 na muuzaji wa duka la dawa baridi wa hapo kijijini kwao aliyejulikana kwa jina la Stephen Ng’wanyi.
Inadaiwa kuwa tarehe 19.07.2016 siku ya Jumanne marehemu alikuwa akilalamika kuumwa na tumbo kwa siku nzima, na ilipofikaJumatano ya tarehe 20.07.2016 maumivu ya tumbo yalizidi, ndipo alipoamua kumweleza ukweli dada yake anayeishi naye aitwaye Anna Fabian kuwa ana ujauzito wa miezi 03 na amechomwa sindano ya kutoa ujauzito na Stephen Ng’wanyi.
Aidha inadaiwa kuwa baada ya hali ya marehemu kuzidi kuwa mbaya, dada wa marehemu Bi Anna Fabian aliamua kwenda kumwita bwana Stephen Ng’wanyi ili aweze kuja nyumbani kwao na kumpatia matibabu mdogo wake.
Bwana Stephen alipofika aliwaomba ndugu zake aondoke na mgonjwa ili akampatie matibabu nyumbani kwake, na baada ya dakika kadhaa alirudi na kuwaeleza ndugu zake kwamba mgonjwa amefariki dunia na baada ya kutoa taarifa alitoroka kusiko julikana.
Jeshi la polisi lipo katika msako wa kuhakikisha mtuhumiwa anayedaiwa kuhusika katika kifo hicho anatiwa nguvuni, huku uchunguzi pamoja na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ukiwa bado unaendelea.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Magu kwa ajili ya uchunguzi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Augustino Senga anatoa wito kwa wananchi hasa wasichana kwamba kutoa mimba bila sababu za kitabibu ni kosa la jinai na kuwashauri kutofanya hivyo.
Aidha wamiliki wa maduka ya dawa baridi wafanye biashara hiyo kwa mujibu wa leseni na taaluma zao na sio vinginevyo
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment