www.kenethngamoga.blogspot.com

Jeshi la polisi Yazuia maandamano ya ukawa

June o7 2016 Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa inayosema kwamba wamepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder)
Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao. Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.

kupitia taarifa hiyo Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia June 07 2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.
Jeshi la Polisi limewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.  Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.
Aidha taarifa hiyo imewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment