www.kenethngamoga.blogspot.com

Vanesa Mdee amponza Bright, aachwa na mchumba wake

Baada ya msanii Bright kuweka wazi hisia zake kwa msanii Vanessa Mdee kuwa anampenda na anataka awe mke wake kwa kumuoa kabisa, kauli hiyo imemtokea puani msanii huyo baada ya binti aliyekuwa na mahusiano naye kumuacha.
Katika story 3 za Planet Bongo ya East Africa radio, amesikika binti huyo akiongea kwa simu na Bright ambaye alirekodiwa bila kujua, na kutoa kauli kuwa hamuhitaji tena aende kwa huyo huyo Vanessa Mdee.
Binti huyo ambaye hatukuweza kupata jina lake alisikika akisema kama hataki tena kuwa na mahusiano na msanii huyo ingawa bado anampenda, na kumtaka akamuoe Vanessa aliyemtaja kwenye media.
Bright ambaye ameachia wimbo wake wa 'Nitunzie' aliomshirikisha Baraka Da Prince, ambao pia ameu-dedicate kwa Vanessa Mdee, hapo jana alifanya interview na Planet Bongo, na kusema hadharani kuwa anampenda Vanessa Mdee, na yuko tayari kufanya chochote ili mradi amuoe awe mke wake rasmi.

Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment