Mamia ya vijana katika jimbo la Bihar nchini India wamelazimishwa kuvua nguo na kubakia na nguo zao za ndani tu ili kuzuia kufanyika kwa udanganyifu wakati wa mtihani wa kuajiriwa kuwa wanajesh
Makuruta wakiwa katika mtihani.
Mamia ya vijana katika jimbo la Bihar nchini India wamelazimishwa kuvua nguo na kubakia na nguo zao za ndani tu ili kuzuia kufanyika kwa udanganyifu wakati wa mtihani wa kuajiriwa kuwa wanajeshi.
Mamia ya vijana katika jimbo la Bihar nchini India wamelazimishwa kuvua nguo na kubakia na nguo zao za ndani tu ili kuzuia kufanyika kwa udanganyifu wakati wa mtihani wa kuajiriwa kuwa wanajeshi.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, picha zimeonyesha vijana wanaowania kuwa wanajeshi wakiwa wamekaa na kukunja miguu katika uwanja mmoja uliopo Mji wa Muzaffar huku wakiwa wamevalia nguo zao za ndani pekee.
Jeshi limesema kuwa lilifanya hivyo ili kuhifadhi mda wa kuwachunguza makuruta wengi huku kuruta mmoja akiliambia gazeti la India Express kuwa alihisi kwamba hawakupewa heshima.
Maafisa wanasema kuwa makuruta wapatao 1,159 walishiriki katika mtihani huo wa saa moja wa kujiunga na jeshi la India.
”Wakati tulipoingia katika eneo la Chakkar Maidan, tuliagizwa kuvua nguo zote isipokuwa nguo ya ndani. Hatukuweza kukataa bali kutimiza yaliyohitajika licha ya kwamba halikuwa jambo la kawaida,”aliongeza Kuruta mwingine.
Makuruta hao walitawanywa kwa urefu wa futi nane kila upande.
Afisa mmoja wa ngazi za juu katika jeshi alinukuliwa na gazeti moja la nchini humo akisema kuwa ni makosa kwa utawala kuwafanyia hivyo makuruta hao.
Bihar na maeneo mengine ya India Kaskazini ni maarufu kwa udanganyifu katika mitihani ambapo mwaka uliopita Serikali ya jimbo hilo iliaibishwa baada ya wazazi na marafiki kupigwa picha wakipanda kuta za shule ili kuwapatia majibu ya mitihani wanafunzi.
BBC
0 comments:
Post a Comment