Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017.

Mbwana Samatta amefunga goli hil kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Farid Musa goli ambalo limedumu hadi dakika 90 za mchezo huo.
Stars imefikisha pointi 4 baada ya kucheza michezo 3, matokeo hayo yanaifanya Stars ifikishe idadi sawa ya pointi na Nigeria ‘The Super Eagles’ lakini Stars ipo mbele ya Nigeria kwa mchezo mmoja. Nigeria itakutana na Misri kwenye mchezo wa kundi ilo siku ya Ijumaa.
Stars itacheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Chad siku ya Jumatatu March 28 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Matokeo ya mechi nyingine za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa mechi ambazo tayari zimemalizika yapo kama ifuatavyo:
Guinea-Bissau 1-0 Kenya
South Sudan 1-2 Benin
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment